Kwa kawaida ungeweza kumuachia mchumba wako suala zima la kukodisha magari ya harusi lakini isipokuwa kama unataka kuvaa vazi lako la harusi na kupanda kwenye gari la harusi ambalo usingelipendelea.
Hivyo ni vyema kuwa na mchango katika kuchagua gari ya harusi katika siku yenu maalum. Kabla ya kuamua juu ya aina ya gari la harusi unalotaka kwa siku yako kubwa, hapa nakuletea mitindo mitano ya hivi karibuni ya gari la harusi
Magari Ya Harusi Ya kisasa
Bado ni chaguo maarufu kwa usafirishaji wa harusi kwani huongeza umaridadi wa siku hiyo, na kawaida huwa makubwa kwa kutosha kuchukua bibi harusi pamoja na bwana harusi. Rangi pendwa za Magari haya ya harusi ni Nyeupe japo kipindi cha hivi karibuni tumeona ongezeko la watu kupendelea gari nyeusi. Magari ya kisasa kama Mercedenz Benz, Range Rover, Hummer na mengine mengi yamekua chaguo kwa maharusi Tanzania
Magari Ya Zamani Ya Harusi (Vintage)
Magari haya sio tu yatakuwahisha kanisani na ukumbini siku ya harusi yako bali yatatia nakshi zaidi katika siku yako hyo. Magari haya yatafanya harusi yako ionekane ya kipekee pia kuongeza vionjo katika picha zako za harusi. Bright Cars tunayo magari haya kama vile Benz Vintage, Nissan Mitsouka, na Benz Classic Vintage
Je Unapaswa kukodisha lini gari la harusi? Jaribu kuchagua na uweke gari lako la harusi angalau miezi minne hadi mitano kabla ya siku yako kubwa. Ikiwa una mahitaji fulani, na unahitaji gari kubwa isiyo ya kawaida, unaweza kuhitaji kuweka mapema kidogo. Utahitaji kutuambia ambao watasafiri kwenye gari, wapi wanahitaji kuchukuliwa kutoka, na wapi wanasafiri kwenda. Tazama Magari ya harusi ya kukodisha kisha bofya hapa kuwasiliana nasi.